Thursday, January 5, 2012

Kirinyaga: Jombi ataka kujitoa uhai baada ya kunyimwa chakula na Mwangi Wilson Murimi

Picha kutoka kwa tovuti
Kalameni mmoja katika eneo la Kirinyaga ya kati aliwashangaza wengi, pale alipotishia kujitoa uhai baada ya mzozo na bibi yake kuhusu chakula kugeukia mweleka wa kifamilia.
Mzozo huo ulianza pale jombi huyo aliporejea nyumbani nyakati za  asubuhi akiwa mlevi chakari, na kudai apewe chakula na mkewe. Hata hivyo bibi yake aliyekuwa amechoshwa na ulevi wa bwanake wa kila siku alimwambia peupe akatafute chakula kwa mama pima. “Nenda ukatafuate chakula huko unakolewa kila siku”, alisema bibi yake.
 Tamshi hilo lilimkera jombi hiyo, aliyemkaba koo mkewe alitumai kuwa hili lingempelekea kuubadili msismamo wako wa awali, lakini kinyume na matarajio yake, mkewe akinyakua ukuni na kumgonga.
Na huku jombi huyo akiachilia shingo yake, mkewe naye alimvamia kwa chochote kilichokuwa pale jikoni, zikiwemo sufuria na vikombe, jambo lililowavutia wanakijiji wengi kujitamazia mweleka wa bure.
Hakuna aliyefanya juhudi zozote kuwatengamisha wawili hao, labda kwa hofu kuwa kufanya hivyo kungeukatisha mweleka huo wa bure ambao ulikuwa ukijiri.
Katikati mwa vurumai hilo, mkewe alisikika akinung’una kuwa mmewe alizoea kutoka ulevini na kulala bila kutekeleza wajibu wake kama bwana. “Mwaname wa saa ngapi huyu, anayejilaza kama mfu?” alisema mwanamke huyo.
Mambo yalizidi unga pale, mwalimu mmjoa wa shule ya msingi kuoka eneo hilo anayedaiwa kuhusika mapenzi kisiri  na mwanamke huyo alipofika pale na kujaribu kuwatenganisha.
Mawazoni pa jombi huyo, wawili hao wakinuia kummaliza ili kupata nafasi kuendeleza uhusiano wao, ndipo akadai kuwa angejitoa uhai. “Kumbe mwatataka kuniua ndio niwaondokee na kumpa nafasi sivyo?” alisema Jombi huyo, “Afadhali nijitoe uhai mwenyewe”
Kicheko cha waliokusanyaika kilikatizwa na mshangao pale bibi yake alipodai kuwa angemhakikishia kuwa amelala pema peponi akijitia kitanzi, jambo ambalo lilimfadhaisha jombi huyo, aliyetoka na kwenda zake akidai kuwa angerejea akiwa mfu.
Mwandishi ni Mwanafunzi katika taaluma ya utangazaji na uanahabari chuoni Maseno na mhariri wa jarida la Equator Weekly

No comments:

Post a Comment